Yanga SCimepanda kileleni mwa msimamo wa ligi kibabe baada ya kuichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Huu ni ushindi wa kibingwa kwa Yanga, kwani wameondoka na alama tatu dhidi ya wapinzani wao Azam Fc ambao hatimaye wameachia usukani wa ligi baada ya kuongoza kwa muda mrefu.
Deusi Kaseke Akishangilia Baada ya Kuifunga Azam fc Goli la Kuongoza
Ni mchezo ambao kocha Cedric Kaze alifanikiwa kimbinu, kwani Yanga ilikuwa hatari sana kila iliposhika mpira.
Bao pekee la ushindi liliwekwa kambani na kiraka Deus Kaseke 'Deda 04' aliyemalizia vyema pasi murua ya Yacouba Sogne
Mpira ulianzia kwa Ditram Nchimbi aliyemsetia Yacouba pasi maridhawa naye kumuwekea katika njia Kaseke.
Yacouba Sogne Akijaribu kuwatoka Mabeki wa Azm fc
Yanga ilikuwa imara zaidi leo eneo la kiungo pamoja na safu ya ulinzi wakifanikiwa kuwadhibiti kabisa Azam Fc ambao walizinduka katika kipindi cha pili.
Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 28 sasa ikikaa kileleni kihalali kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya Azam Fc na alama tano dhidi ya Simba.
Tuisila Kisinda Akimtoka Mchezaji wa Azam fc,
Ni mwendo wa rekodi kwa kocha Kaze kwani kikosi chake hakijapoteza mchezo wowote msimu huu
Yaani Yanga haijafungwa kabisa iwe kweye ligi au mchezo wa kirafiki. Wananchi wana kila sababu ya kutamba kwani msimu huu unaweza kuwa na furaha kwao.
0 Comments