Kiungo fundi wa Yanga Mapinduzi Balama atarejea nchini leo Ahamisi akitokea Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Nyota huyo alifanyiwa upasuaji wa goti wiki iliyopita na sasa akitarajiwa kurejea dimbani baada ya kupona.Madaktari waliokuwa wakimtibu, wameuhakikishia uongozi wa Yanga kuwa nyota huyo hatakuwa na changamoto zaidi na watarajie ataweza kuungana na wenzake kuendelea na majukumu yake pale atakapokuwa amepona.
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga ambao hawajamshuhudia nyota huyo dimbani kwa takribani miezi saba.

0 Comments